Luke 22:47-53

Yesu Akamatwa

(Mathayo 26:47-56; Marko 14:43-50; Yohana 18:3-11)

47 aYesu alipokuwa bado anazungumza, umati mkubwa wa watu ukaja. Uliongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili. Akamkaribia Yesu ili ambusu. 48Lakini Yesu akamwambia, “Yuda, je, unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?”

49Wafuasi wa Yesu walipoona yale yaliyokuwa yanakaribia kutokea, wakasema, “Bwana, tuwakatekate kwa panga zetu?” 50 bMmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume.

51Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa lile sikio la yule mtu na kumponya.

52 cKisha Yesu akawaambia wale viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu, pamoja na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba mimi ni mnyangʼanyi? 53 dSiku kwa siku nilikuwa pamoja nanyi Hekaluni lakini hamkunikamata. Lakini hii ni saa yenu, wakati giza linatawala!”

Copyright information for SwhNEN